t

Update

TERMS AND CONDITIONS

Welcome to our website. If you continue to browse and use this website, you are agreeing to comply with and be bound by the following terms and conditions of use. If you disagree with any part of these terms and conditions, please do not use our website.

The use of this website is subject to the following terms of use:


You may not do any of the following while accessing or using the Inclusive Development for Citizens platform and services:


Uwepo wa sheria ni muhimu katika kuhakikisha watoto waliopata Mimba wakiwa shule wanapata nafasi ya kupata elimu katika mfumo Rasmi baada ya kujifungua:

Elimu ni suala la muhimu katika maendeleo ya nchi yetu, Ili kuwasaidia wanafunzi kufikisha malengo hayo ni lazima kutengenezwe mazingira mazuri yasiyo na vikwazo ili kuwawezesha wanafunzi kufurahia elimu yao. Mazingira ya sasa yana changamoto nyingi sana hasa dhidi ya watoto wa kike, Pamoja na jamii kuwa na mwamko mdogo katika kupatia watoto wa kike elimu, kuna vikwazo ambavyo vinatokana na sera au mitazamo ya viongozi , moja ya suala hili ni pale mtoto anapopata mimba akiwa na umri mdogo.

 

Saikolojia ya mwanafunzi inapaswa kwa kiasi kikubwa izingatie katika elimu kama msingi mkuu, ili wasiwaze suala lolote ambalo linaondoa umakini wao katika masomo na ukuaji kama watoto, kuna mambo ambayo yanawakabili wanafunzi hasa watoto wa kike ambayo ni magumu na nje ya uwezo wao kama wanafunzi lakini pia kama Watoto wadogo wanaotegemea jamii iwalinde na kuwasimamia katika kutafuta mafanikio yao ya baadaye.

 

Hata hivyo ni vyema kuangalia sheria na sera zetu kama zitasaidia mwanafunzi kutimiza haki hiyo ya msingi ya kupata elimu pasipo vikwazo, sheria ni tegemezi kubwa la Watoto wa kike ambao wamepata ujauzito wakiwa bado ni wanafunzi ili kutoa mwongozo wa namna gani wanaweza kuendelea na masomo hasa baada ya kujifungua. Lakini pia kuzingatia kwamba mtoto aliyepata ujauzito anapoondolea shule na kisha kurudishwa baadaye suala lake la mimba lisiwe gumzo kwa wanafunzi wengine, hivyo wakati wa kuwarudisha ni muhimu kufanya uchambuzi ni arudishwe shule gani, ile ile au shule nyingine na kwa utaratibu upi. Tunapaswa kutoa mwongozo na sheria ambayo itaondoa vikwazo kwa mtoto wa kike akipata ujauzito kutoendelea na masomo katika mfumo rasmi hasa kwa shule za umma ambazo hutegemewa zaidi na watoto kutoka katika familia zenye uwezo mdogo kifedha.

 

Kuweka utaratibu mzuri wa sheria na sera kutasaidia kupunguza kwa kiasi kikubwa utegemezi wa vijana wengi katika jamii hapo baadaye, kwani wanafunzi ambao wanapata ujauzito huishia kuacha shule na kuwa wategemezi kwa familia zao hivyo kuwa mzigo katika maendeleo ya familia kwa kiasi kikubwa. Mfumo wa masomo ya ufundi sio mfumo sahihi, hivyo sio sawa kuwatumbukiza huko wanafunzi wote wanaopata ujauzito. Wanafunzi wenye nia na uwezo wa kuendelea na masomo wasiwekewe kikwazo cha kusoma masomo ya ufundi tu ambayo kwa kiasi kikubwa yanaondoa fursa nyingi za ajira hapo baadaye, lakini pia yana vikwazo vingi katika kuendelea na elimu ya juu ikilinganishwa na mtoto anayesoma katika mfumo rasmi. Kuwanyima watoto wa kike elimu ni ubaguzi mkubwa sana wa kijinsia Mtoto wa kike anastahili uhuru kwa kiasi kikubwa katika kupata elimu ili kujenga jamii iliyo bora kwani Taifa linapowekeza katika elimu kwa watoto wa kike linajenga na kuimarisha kizazi cha sasa na cha baadae.

 

MWISHO NA MUHIMU: Kama jamii tuna wajibu wa kupambana na sababu zote zinazosababisha ujauzito kwa watoto wa kike wakiwa shuleni, pamoja na umuhimu wa kuondoa kikwazo cha kuwanyima elimu pale wanapopata ujauzito tunatakiwa kuzingatia pia malezi ya watoto wa kike ili wasijikute kwenye janga hili la mimba za utotoni.

#ArudiShule #ElimuBilaUbaguzi #ActiveCitizens


download REPORT Posted on : 03 June, 2022